UNAMSHANGAA NYANI ALBINO!
Ni aghalabu sana viumbe kama hawa kupatikana kirahisi, pichani ni Nyani aina ya Albino ambao ni adimu kupatikana katika misitu mbalimbali iliyopo ndani ya Taifa hili lenye upendo, Amani, sambamba na utulivu, upatikanaji wa nyani huyu ulichukua muda mrefu kwani kazi hiyo ilifanywa zaidi na mizimu ya Dr. Manyaunyau baada ya Babu Alola kutoa maelekezo ambapo mahali angeweza kupatikana nyani huyu albino, Nyani huyu alipatikana katika maeneo ya Chole Kisemvule huko Kisarawe licha ya watu wengi kudai kuwa viumbe hawa hawapo hapa nchini na kudai kuwa hupatikana katika mabara ya Asia, lakini ukweli ni kwamba nyani huyu ameopolewa katika moja ya misitu ya Tanzania na ni hapahapa Kisarawe mkoa wa Pwani.
0 comments:
Post a Comment