Wednesday, July 28, 2010

JICHO LAGU LEO





KARIBUNI KWENYE LIBENEKE LA DR.MANYAUNYAUNa Baraka MfunguoAfrika tuna utamaduni wetu ambao tumeurithi kutoka kwa mababu zetu. Mababu zetu waliishi kulingana na miiko iliyoendana na maadili kadiri ya wao walivyorithi kutoka kwa waliowatangulia. Katika hayo yapo mambo mengi kama vile jando na unyago, Utani,Ngoma za jadi, Utambaji wa hadithi za kale, Utabiri wa nyota nk nk. Katika hayo pia yapo matambiko mbalimbali yaliyotumika kuwaomba mizimu mambo mbalimbali endapo jamii itakuwa imekwenda kombo.Leo hii ukitembelea Tanzania waweza shuhudia maajabu ya kutisha mfano Msitu mkubwa wa Ngende uliopo mkoa wa Lindi, Hifadhi ya viboko ambao huombwa kupitia lugha za mizimu kabla ya kwenda kuwatembelea ili wasikudhuru hawa wako rufiji, Mapango ya Amboni Tanga, na eneo la Mashe mkoani Kilimanjaro. Pamoja na maeneo mbalimbali ambayo sikuyataja. Amini usiamini hii ndio Afrika.Hivi sasa yupo kijana mahiri ambaye amejitolea kupambana na nguvu za giza kupitia tiba asilia na mizimu anayeitwa Dr Manyaunyau natumaini watu wa mkoa wa Dar es Salaam wanamfahamu vizuri. Dr Manyaunyau ameanzisha libeneke lake ambalo anakwenda kukujuza yale ambayo yanatukia ili wewe msomaji pale ulipo ujue kwamba Waafrika bado tunatisha kwa ile teknolojia yetu ambayo hata mzungu haoni ndani. Kimsingi huu ni ujasiri mkubwa kwani kwa kufanya hivyo Dr Manyaunyau atakuwa amepanua wigo mkubwa wa watu kufahamu kazi zake, kujenga mahusiano mazuri, kuwasiliana, na kupanua biashara zake. Blogu hii inampongeza Dr Manyaunyau kwa uamuzi wake wa busara wa kuanzisha libeneke lake.Ikumbukwe miaka ile ya zamani alikuwepo mzee mmoja aliyeitwa Tekelo ambaye alikuwa anatisha katika fani hii ya kiafrika nami napenda kuifananisha staili hii na ya Dr Manyaunyau kiboko ya wachawi. Ninamtakia kazi njema Dr Manyaunyau pamoja na libeneke jema

0 comments:

 
Design by Kwetu Bongo