Thursday, May 27, 2010

Hausigeli azua balaa Dar
Wednesday, 05 May 2010 13:11
*Adaiwa kuweka sumu kwenye chakula *Familia nzima ipo hoi hospitali *Atoweka, Polisi wamsaka
Na Saida Said, jijini
WATU watano wenye asili ya Kihindi wamelazwa katika Hospitali ya Burhan jijini wakiwa wamepoteza fahamu baada ya kula chakula chenye sumu inayodaiwa kuwekwa na msichana wao wa kazi za ndani.
Watu hao ni Nasrim Mohamed (28), Nafra Azran (20), Mohamed Majid (32), Azran Jeward ambao ni mke na mume pamoja na mgeni wao, Abdallah Mohamed (40).
Akizungumza na Mwandishi wa gazeti hili, ndugu wa karibu katika familia hiyo ambaye ni dada wa mmoja wa wagonjwa hao, Parin Adam, amesema tukio hilo limetokea Mei 3 mwaka huu, saa 3 usiku, Kariakoo.
Amesema dada yake Nasrim anawafanyakazi watatu wa ndani ambao, kati ya hao, wawili wanalala hapo hapo na aliyepika chakula hicho ni yule anayekwenda kufanya kazi na kuondoka.
Amesema hali ya wagonjwa hao ilianza kubadilika baada ya kula chakula cha usiku ambapo walipoteza fahamu na kuibiwa vitu vyao vya thamani zikiwamo fedha, simu za mkononi na dhahabu ambazo walivuliwa na msichana wa kazi aliyemtaja kwa jina moja la Hadija.
Alisema wanaamini kuwa Hadija ndiye aliyeweka sumu hiyo kisha akatoweka.
Ilipofika asubuhi, msichana mwingine wa kazi alijaribu kuwaamsha mabosi wake bila mafanikio, ndipo alipopiga simu kwa baba wa Nasrim wakaenda kuwachukua na kuwakimbiza hospitali ya Ibrahim Haji, iliyopo Posta.
Amesema baada ya muda, waliambiwa wawataoe wagonjwa wodini kwani wao wanataka kuwalaza wagonjwa wengine, hivyo walilazimika kuwahamishia katika Hospitali hiyo ya Burhan.
Akizungumzia hali ya wagonjwa hao, muuguzi katika hospitali hiyo, Nasma Wasta, amesema wanaendelea vizuri kwani walifikishwa hospitalini hapo wakiwa hawajitambui.
“Hali zao zinaendelea vizuri. Walifikishwa hapa wakiwa wamepoteza fahamu lakini hivi sasa, fahamu zimeanza kurudi ingawa hawazungumzi vizuri,” alisema Wasta.
Amesema hadi sasa bado haijajulikana ni kitu gani walichokula ambacho kimewafanya wafikie hali hiyo kwa kuwa majibu ya daktari bado hayajatolewa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile amesema kuwa............

0 comments:

 
Design by Kwetu Bongo