Sunday, June 27, 2010

KUPATA MTOTO WA DHAHABU

DHIKR NA DUA TOKA KATIKA QURAAN NA SUNNAH KWA WAJAWAZITODhikr and dua ihizi ni kutoka katika kitabu Al-Ifadagh fi Ma Jaa fi Wirdi’I-Wiladah (Indonesian edition, Smart Media, 2006)
Kilichoandikwa na Nurah binti ‘Abdurrahman, mwanachuoni mkubwa wa kike akielezea umuhimu wa dhikr wakati wa ujauzito au kwa apangaye kupata mtoto , kupunguza machungu ya uzazi na kuwepesishia uzazi kwa dhikr na dua.

Dua hizi pia hufanya mtu kupata motto mwema, mchamungu, mwenye kipaji cha kushika masomo na kuhifadhi na mtiifu mbele ya Mungu na wazazi wake wawili na wakubwa kwa ujumla.Dua hizi zina nguvu za kumlinda mzazi na motto dhidi ya majanga ya uchawi, kijicho na hasadi, kurogwa au kutupiwa majini au kukumbwa na mapepo .

Inapendeza kusoma au kusomewa mtarajiwa, vilevile si vibaya ayah hizi na sura hizi au dua zikiandikwa kwenye karatasi kwa wino wa zaafani akawa mama mja mzito anatumia kunywa na kujipaka mwilini.Pia ayah hizi zikisomwa katika mafuta ya zaytuni yalochanganywa na mafuta ya misk na ambar mtumiaji akawa anajipaka baada ya kuoga wakati wa usiku tu.
Aya hizi na sura hizi zinaweza kurekodiwa kwenye simu au MP3/4,CD , Kaseti nk na mzazi akawa anazisikiliza mara kwa mara.

Mpango huu wa Dua unaweza kufanywa na wale wenye kutaraji kuoa au kuolewa na wale ambao hawajabahatika kupata mtoto/watoto.Inajuzu pia kuwasikilizisha watoto wakati wa kulala na hata kuwahifadhisha watoto dua hizi kwani zina siri kubwa mno kujenga tabia njema, utiifu , adabu na kuwafanya kuwa watoto wema.


Mbali na dua ili kupata mtoto mwema, mwenye akili, bidii na kujituma, yapo mfundisho maalum ya kumfanya mtoto awe mwema na kadhalika.Lakini mafundisho mema na mazuri huanza mtoto akiwa tumboni mwa mama yake, je hili ulikuwa unalijua ndugu yangu?Kithirisha Sana kufanya Istighfaar (Astaghfirullah) kwani kuna wepesi katika kila jambo gumu na zito


Muelekee Mola wako kwa akili , mwili na roho yako kwa dhaati kabisa na uamini Nguvu Kuu ya Ki-Mungu katika utendaji wa Dua na maombi kupitia Quraan , Dhikr na Dua . Kuwa na yaqini kuwa yale uyaombayo na umuelekeapo Allah utayapata bi-idhni-Llah.
Quraan huleta utulivu wan yoyo na raha isiyo kifani, anasema Allah aktika Quraan tukufu


28.Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua!


29.Wale walio amini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri.

Quraan Surah Ar-Ra’d: 28-29Dhikr/Uradi kwa mama Mjamzito au anayepanga kupata ujauzito

1.surah Al-Fatihah Ayah 1-7 Rudia mara saba
2. surah Al-Ikhlas Ayah 1-4, Rudia mara tatu
3. surah Al-Falaq Ayah 1-5mara tatu
4. surah An-Naas Ayah1-6, mara tatu
5. Al-Baqarah 255(Ayat Kursiyu), mara tatu au mara saba
6. mwisho wa surah Al-Baqarah(Amana Rasulu):Ayah 285-286, mara moja
7. mwanzo wa surah Al-Baqarah:Ayah 1-5, mara moja
8. surah Al-Hashr:Ayah 22-24,mara moja
9. surah Twaha: Ayah111, mara moja
10. surah Al-Anbiya’:Ayah 69, mara tatu
11. surah Al-An’am: Ayah17, mara tatu
12. surah Al-Isra:Ayah 82, mara tatu
13. surah At-Taubah: Ayah14, mara tatu
14. surah Yunus: 57,Ayah mara tatu
15. Mwisho wa surah An Nahl:Ayah 68, mara tatu
16. surah As-Shu’ara’: Ayah80, mara tatu
17. surah Fussilat: Ayah44, mara tatu
18. surah Al-Qalam:Ayah 51, mara tatu
19. surah Yaasin:Ayah 9, mara tatu
20. surah Al-Zilzalah: Ayah1-8, mara saba
21. surah Al-Inshiqaq:Ayah 1-4, mara moja
22. surah Al-A’raf: Ayah 54-56, mara moja
23. surah Yunus: Ayah 3, mara moja
24. surah Al-Kaafirun: Ayah1-6, mara moja
25. surah An-Nasr:Ayah 1-3, mara moja
26. surah An-Anazi’at:Ayah 46, mara tatu
27. surah Al-Ahqaf: Ayah35, mara tatu
28. surah Al-Anbiya’: Ayah83, mara tatu
29. surah Al-Anbiya’:Ayah 87, mara tatu
30. surah Al-Muumin:Ayah 44, mara tatu
31. surah Al-Qamar: Ayah10, mara tatu
32. surah Huud: Ayah88, mara tatu
33. surah Ali Imran:Ayah 173mara tatu
34 surah At-Taubah: Ayah129, mara saba
35. surah At-Talaq: Ayah3, mara saba
36. surah Al-Mu’minun:Ayah 97-98, mara tatu
37. surah Al-Mu’min: Ayah1-3, mara moja
38. surah Nuh:Ayah 10-12, mara moja
39. surah Al-Fajr: Ayah27-30, mara moja
40. surah As-Saffat Ayah1:10, mara moja


Zingatia:Mbali ya sura hizi ongezea kusoma surah Maryam, Qaf, Al-Fath,Surah Yaasin na sura Al-Mulk zisomwe mara moja kila surah yapendeza zikirekodiwa kusikilizwa kwenye simu, MP 3/4 na vifaa vingine vya kusikiliza.Inaathari ya ajabu unaposikilizia sikioni.

Ziada katika hili jitahidi kukhitimisha Quraan kwa kusoma au kusikiliza angalau kila baada ya siku kumi kwa kipindi hiki cha ujauzito na kipindi cha miaka miwili ya malezi ya mtoto


DUA ZA KUSOMA WAKATI WA UJAUZITO/UNATARAJI UJAUZITO AU KUOA/KUOLEWA NA WANAWARI

Wakati wa ujauzito, duas za kujilinda dhidi ya mabalaa zisomwe kwa wingi, kujipinda kwenye ibada kuwe kwingi mno na kuswali kwa wakati
Mfano wa dua na sura hizo ni kama ifuatavyo

A'udhu bikalimmatillaahit taammmaati min sharri maa khalaqa

Hasbunallaahu wa ni'imal wakiil

Inniy u'iidhuhaa bika wa dhurriyyatahaa minas shaytaanir rajiim


Aayatul Kursi, surah Yasin, surah Maryam, surah Yusuf na surah Muhammad zisomwe

Imesimuliwa kuwa Sayidah Fatimah Zahrah (radiyallahu anha) ilipokuwa inafikia wakati wake wa kuzaa, Mtume Sallallahu alayhi wasallam alikuwa akimuagiza Umm Salma (radiyallahu anha) na Sayidah Zainab (radiyallahu anha) na maelekezo ya kumsomea
Aayatul Kursi, surah Al-Falaq na Surah An-naas na Ayah zifuatazo kuwepesisha mazazi

Inna rabbakumullaahul ladhiy khalaqas samaawaati wal ardha fiy sittati ayyaamin thumma-stawaa alal arsh, yughshiyl llaylan
nahaara wa yatlubuhu hatheethan was shamsa wal qamara wan nujuma musakh-kharaatim bi amrihi. Alaa lahul khalqu wal amru,
tabaaraka llaahu rabbul aalameen. Ud'uu rabbakum tadharru'an wa khufyatan, innahu laa yuhibbul mu'tadiin.

Surah Al-A'raf (7:54,55)

Ikiwa mwanamke ana ugumu wa kuzaa au ana matatizo wakati wa kuzaa , andika ayah hiyo

hapo juu kwenye karatasi safi na ikunjwe kwenye kitambaa cheupe , amfunge pajani kwake

kurahisisha mazazi Insha-Allah atamuwepesishia uzazi

Vilevile Aayatul Kursi na Ayah mbili toka surah Al-A'raf (7: 54,55) zisome wakati mama

mjamzito anakaribia kuzaa vilevile Surah al Falaq na Surah An-Naas zisomwe na kumpulizia mzazi mtarajiwaDHIKR YA MAJINA YA ALLAH YASOMWE WAKATI WA UJAUIZTO NAYO NI KAMA IFUATAVYO:-

Yaa waahidul ahad,

Yaa awwalu mara arobaini kila siku

Yaa mubdi-u, Mara 99 jina hili huzuia utokaji wa mimba (Insha-Allah)

Yaa barru, Mara 7

Yaa baari-u, mara 21

Yaa musawwiru, mara 21

Yaa naafi-u, mara nyingi na inapendeza kusema jina hili kabla ya mke na mume kuingiliana

Na kusoma majina yote 99 Inapendeza zaidi kipindi hikiKithirisha kusoma Dua hizi kwa wingi

1.Allahummâ Lakal Hamdû Wa Lakash-Shukru

2. Jizoeshe kufanya Naafil(Sunnah) kila mara na usome Dua hii katika sijidah

Rabbi Hab Liy Min-Ladunka dhurriyatan-Tayyibah Innaka Sam'iud-Du'aa

3. Rabbi-j'alniy Muqiima-Swalaati wa min dhurriyatiy Rabbanaa wa Taqabbal Du'aa4Kuwa mwepesi wa kusamehe na kufanya Istighfaar kwa wingi, jitahidi kujisomea habari za kidini zaidi hususan zile zenye kukupelekea kuwa mcha mungu na habari za pepo na jaribu kuwa mchangamfu na mwenye furaha wakati wote. Kuwa mkimya na achana na mizozo isyojenga na kuwa mwenye kuomba msamaha wakati wote, usikorofishane na mama mkwe au mawifi na jamaa wa karibu na hata wa mbali.Magomvi huwa yanaathiri watoto walio matumboni mwa mama zao hata wale ambao waliozaliwa wakiona magonvi huwaathiri na tabia hizi huwa zinaendelea na watoto kuwa wakorofi na wagomvi.
Fanya kuwa karibu na Mola wako haya yatajenga mapenzi makubwa baina ya mja na mola wake.
Wacha kuwa na tabia ya usengenyi (Ghiba), choyo, kibri na uvivu.kuchunguza maisha ya watu na mengineyo mfano wa hayo.

Kumbuka , kipindi hiki cha ujauzito wewe hauko pekee yako ila una kiumbe umekibeba na kiumbe hiki kinategemea zaidi ulaji wako(lishe yako), fikra zako, utashi wako , tabia zako.Mtoto huyu atakuwa na tabia njema iwapo wewe utakuwa na tabia njema kipindi hiki cha ujauzito, atakuwa mnyonge endapo wewe utakuwa mnyonge kipindi hiki cha ujauzito na hali hii haitoweza kubadilika baada ya mtoto kuzawa(kuzaliwa).Mtoto huyu atakuwa mchamungu, mwenye akili , mwerevu, mwenye kupenda dini yake ikiwa wewe utazibeba hizi tabia na atakuwa kinyume chake pale utakapobeba tabia hizi.Kuwa makini kwa chakula chako na tabia zako kipindi hiki, acha kulalamika bila kipimo kuwa mtu wa kushukuru na usipende kuwa mbishi kwa kila jambo.

1.Chunga diet yako .Hakikisha unatafuna chakula kabla ya kukimeza kwani inaweza kukuletea kiungulia na zingatia usile ukavimbiwa.

2.Jitahidi kula mbogamboga kama vile Salad, mchicha, kisamvu , matango kwa wingi , hakikisha unayaosha kabla ya kula

3Kunywa maziwa kwa wingi .Maziwa yana virutubisho vingi , baada ya kula vyakula vingine Mtume S.A.W alikuwa akisema(akiomba Dua) Allahummâ At'imnâ Khayran-Minhu
Wakati alipokuwa akinywa maziwa au akipewa maziwa alisoma Du'aa ifuatayo :
Allahummâ Bârik Lanâ Fîhî wa Zidnâ Minhu

Kwa maelezo mengine ni kusema Mtume wetu S.A.W hakuomba zaidi kama alivyoomba wakati wa kula chakula (kupewa chakula) kwa sababu hakuna chakula kizuri kuliko maziwa (kwa virutubisho) kiufupi mama mja mzito anywe maziwa kwa wingi kipindi hiki cha ujauzito kwani kuna vtamini nyingi na protein zinazohitajika kwa mwanadamu kama maziwa ya kawaida ya atahri kwa kwako basi jitahidi kutumia bidhaa zingine zenye maziwa kama vile maziwa mgando , custard na kadhalika kwani ni faida kubwa kwa mama na mtoto

4Jitahidi kujiweka mbali na unywaji wa chai au Kahawa, mafuta yatokanayo na wanyama maka vile samli, pilipili, na chakula cha mafuta mbali na kuwa atahri katika mfumo wako wa chakula vyakula hivi vina madhara kwa misuli na mishipa ya fahamu
6. Jaribu kuwa mbali na mume kwa miezi mitatu ya mwanzo na miezi mitatu ya mwisho hususan kuanzia mwezi wa saba na kuendelea kwani kipindi hiki mzazi anakuwa taabani Ki-Psycholojia na motto tumboni huweza kudhurika.

7. Jitahidi kulala mapema .Usilale kwa masaa mengi jaribu kulala angalau kwa masaa manane , hii hufanya akili yako na aili ya mtoto kupata utulivu

8.Jitahidi kuacha kufanya kazi ngumu kwani hii inaweza kusababisha mimba kutoka


Kwa wale wafuatao Twariqa wawasiliane na Sheikhe(Murshid) kwa muongozo zaidi wa

Kitwariqa ila mnaweza kuongezea Hizbu Bahar , Hizbu Nasr na Hizbu Ayat za Imam

Abal Hassan As-Shadhuli pamoja Wadhifa al Mashish/Swalat Mashishiyah kama ilivyo

maelekezo ya Twariqa Shadhiliyah ,Hizbu Ghazali kwa maelekezo ya Twariqatul Qadiria, Wasilatu Shafiy, Swalat Nariyah, na visomo vingine vya Kitwariqa kama utakavyoelekezwa na Sheikhe au Khalifah wako wa Twariqa unayoifuataUnaweza kuhudhuria Dhikr za pamoja ila kwenye hadhara ushiriki wako uwe kwa pembeni kutokana na nguvu itumikayo kwenye Hadhara ni kubwa inaweza kusababisha maumivu au madhara ya kiumbe ulichokibeba.Kumbuka kiumbe kicho tumboni kwako kinasikia na kushiriki haya yote na utaona ajabu atakapozaliwa akiwekewa CD au kusikia sauti za Quraan , dhikr na visomo vingine utaona maajabu respond yake inavyokuwa.

Zaid ya maelekezo hayo tuliyoyatanguliza, mazingatio mengine ya msingi na fadhilat za mama mjamzito na mzaziONGEZA IBADA
Dua ni mahusiano baina ya mja asiye na nguvu wala uwezo wowote na Mola wake mwenye nguvu kuu, mwenye uwezo wa kubadilisha chochote na wakati wowote bila ya kutegemea kitu chochote ambaye ni Mola wa viumbe wote.Dua zina nguvu sana kwa kina mama wakati wa ujauzito wao na hata kwa watoto wao.Hii haina maana mume naye asishiriki katika kuomba Dua na kusoma Quraan, bali wote washirikiane kwa pamoja nah ii huleta mapenzi na mshikamano wa kifamilia.
Dua huombwa ili kuondoa unyonge, dhiki, shida , matatizo, maradhi na kuondoa mabalaa na mambo mengi.Pia Dua hufanywa ili kuomba kupata mtoto mwema, mtiifu, mwenye adabu, mwenye akili na asiyekuwa na choyo wala ubaguzi.


Katika dua kubwa za kuomba mtoto mchamungu na mwenye kuleta furaha na faraja kwa wazazi wake ni dua hii

Rabaan Hablana min azwajina wa min dhurriyatina qurrata a’ayunin waja’alna lilmutaqina imama

Na wale wanao sema: Mola wetu Mlezi! Tupe katika wake zetu na wenetu yaburudishayo macho, na utujaalie tuwe waongozi kwa wachamngu
Surah Al-Furqaan: 74:

Pia Dua ya kuomba wakati wazazi wanafanya jimai ili shetani asiwakaribie ambayo ni Allahuma janabna shayatwin maa Razaqnaa· VISIMAMO VYA USIKU (QIYAMU LAYL)
Swala za usiku hususan katika masaa mazito ya usiku ni njia muafaka ya mja kuwa karibu na Mola wake na Mola humpa mja wake alitakalo kwa wakati huo muafaka.Ibada hizi huongeza uchamungu, wengi hupata daraja la uwalii(wilayah), nguvu za kiroho kupambana na nguvu za kishetwani/iblis aliyelaaniwa, nguvu za kiroho kupambana na matamanio ya nafsi na imani hupanda sana kwa kufanya ibada za usiku

· Ongeza kusoma Quraan
Watu wa Ilm Nafsia (Psychology) wanatueleza kuwa kuanzia kipindi cha wiki 20 ya ujauzito mtoto aliyeko tumboni huweza kusikia sauti nje ya tumbo, na sauti hizo huweza kumuathiri mtoto, ikiwa ni sauti za kuleta furaha basin a mtoto atakuwa ni mwenye furaha na ikiwa ni sauti za huzuni au matusi au kukaripia basin a mtoto ataathirika kama anavyoathirika mama.Hivyo sauti nzuri ya mtoto kusikia ni sauti ya Quraan ikisomwa
Mwenyezi mungu anasema katika Quraan

‘’…Na kumbukeni yasomwayo majumbani mwenu katika Aya za Mwenyezi Mungu na hikima. Kwa hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa mambo ya siri, na Mwenye khabari.. Surah Ahzab ayah34

Kusoma Quraan kunaleta amani, utulivu , kuongeza imani vilevile kwa yule anayeisikiliza Quraan hupata utulivu na amani hii.Wanawake wajawazito wanahitaji utulivu na amani hii wakati wa ujauzito na hata wakati wa malezi ya watoto na kunyonyesha.Vipindi hivi huwa vigumu mno kisaikolojia kwa wanawake, hivyo wanahitaji msaada wa ziada ambao ni Dhikr, Quraan , Dua na Ibada kwa wingi.

Kwa mtindo huu wa kusoma na kusikiliza Quraan humuambukiza mtoto aliyeko matumboni mwa mama yake na huwa rahisi mno kusoma Quraan kwa kuisikia tu ikisomwa na haisahau maishani mwake kwa idhni ya Mungu na kujenga mahusiano ya karibu mno na Quraan na ibada.Kama tulivyoongea hapo juu jitahidi kukhitimisha Quraan kila baada ya siku tatu au siku kumi kwa kusoma au kusikiliza.Inshallah Allah atakujaalieni maisha yaliyo bora kabisa

FADHWILA NA MALIPO UJAUZITO/UZAZI
Mtume Sallallahu alayhi wasallam anasema: "Mwanamke akifa ilhali bado ni mwanamwari (bikrah) au wakati wa ujauzito au wakati wa uzazi atakuwa amefikia darja ya shuhada (shahidat)
Imesimuliwa kutoka kwa Mtume Sallallahu alayhi wasallam kuwa : "Je haikutesheni kwenu nyie wanawake kuwa pale mnaposhika mamba za waume zenu na mumeo akaridhia juu ya jambo hilo jema ya ujauzito basi mtapata malipo sawa na mtu aliyefunga kwa ajili ya Allah
Na mtu huyo ni mwenye kusmama kisimamo cha usiku huku mchana wake amefunga, na mnapokuwa kwenye uchungu wanadamu, majini na malaika huwa hawajui zawadi nono uliyooandaliwa na mola wako(ni zawadi bora mno) na anapozaa na kuanza kumnyonyesha mtoto basi kila fundo la maziwa anyonyae mtoto unakuwa unalipwa na unapokuwa macho usiku kwa masumbufu ya mtoto basi unalipwa malipo sawa na mtu aliwacha huru watumwa sabiini kwa ajili ya Allah Ewe Salamah !Je unawajua wanawake hawa?Ni wanawake wacha Mungu, wenye kuatii waume zao, na si wajeuri kwao


Mtume Sallallahu alayhi wasallam asema "Mwanamke mjamzito mpaka wakati wa kuacha kunyonyesha anakuwa ni sawa na askari wa Kiisilamu anayelinda ngome ya Waisilamu isivamiwe na akifa katika kipindi hiki basi anakuwa amekufa shahid

Katika Hadith nyingine inasimuliwa kuwa Mtume S.A.W anasema kuwa , mwanamke akifa katika muda wa kuzaa basi anakuwa amekufa shahid (shahidah)."

Hadharat Mail bin Yasaar (radiyallahu anhu) anasimulia kuwa Mtume Sallallahu alayhi wasallam anasema : "Oeni wanawake ambao ni wazuri na wenye kizazi kingi kwa sababu siku ya Qiyama nitakuwa ni mwenye kujisifu kwa kuwa Umman wangu ni mkubwa


Katika Hadith nyingine Mtume Sallallahu alayhi wasallam anasema : "Hata mimba iliyotoka ilikuwa ya miezi miwili au mitatu , basi hicho kiumbe kitamkokota mama yake kwenda peponi , ikiwa huyu mama alikuwa na subrah na matumaini ya kulipwa ujira mwema toka kwa Allah

Mtume Sallallahu alayhi wasallam anasema : "Mwanamke anayenyonyesha hulipwa kwa kila fundo analonyonya mwanawe , na malipo yake ni sawa na kufanya uponyo au kumpa uhai mwanadamu mmoja au kuokoa maisha ya mwanadamu kwa kila fundo la maziwa atakayompa mwanye na anapomuachisha mtoto wake basi Malaika huwepo na kumpa hongera na huku wakisema Mabruk…Mabruk , Madhambi yako yote yaliyopita yamesamehewa na sasa unakuwa kama vile unaanza upya!Na dhambi hapa iongelewayo ni madhambi madogomadogo na si madhambi makubwa.


Allah ndiye mjuzi wa kila kitu

0 comments:

 
Design by Kwetu Bongo