Tuesday, June 1, 2010

KUTIBU UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Kutibu upungufu wa nguvu za kiume au kupungua hamu ya kujaamiana baina ya mke na mume
Kupungua Nguvu za kufanya mapenzi ziko za aina mbili
1. Mume kutokuwa na nguvu za Kiume(kutosimamisha uume au kutokuwa na nguvu ya kuendelea kufanya jimai)
2. Mke kutokuwa na hamu ya kufanya jimai na mumewe au kusikia machungu wakati wa kujamiiana na mumewe
Dalili zinazofahamika ni kuwa maumivu juu ya mapaja , kusikia uzito wa kichwa na kuumwa kichwa mara kwa mara na pia hali ya kimawazo kubadilika badilika kila mara(hasira na mchangnanyiko wa mambo)

Tiba
Andika Ayah hizi kwenye karatasi safi na uzisomee hizo karatasi zikiwa ndani ya maji sura zifuatazo

Al-Fatihah 1:1-7 mara saba
(Ayat Al-Kursiy 2:255
Yunus 10:81-82
Twa-Ha 20:69
Sura za kujilinda na mabaya (Al-Ikhlaas 112, Al-Falaq 113, An-Naas 114)

Mgonjwa akoge, anywe na kujipaka maji haya kwa muda wa siku saba mpaka siku ishirini na moja.Na pia asome aya za kubatilisha uchawi kama tulivyotanguliza kuzisema hapo mwanzo(makala iliyopita dalili za kupatwa na majini) na ajipake kwenye mapaja na atumie mafuta ya Zeituni (Aya hizi ziandikwe kama kombe na kuwekwa kwenye mafuta ya Zaituni na zisomewe tena hizo aya kwenye mafuta hayo)
Kinywaji kilichotengenezwa kwa mchanganyiko wa Habat sawdah, asali , ndimu , tangawizi na pilipili mtama kinywaji hichi kisomewe ayah hizo hapo juu na aya za kubatilisha uchawi(Ibtwaru Sihr) na mgonjwa anywe asubuhi , mchana na jioni.kinywewe kama chain a unaweza kukitengeneza kwa majani ya chai au kahawa.
Mgonjwa atumie mafuta mazuri, hususan Misk na wakati wa kulala ajipake hiyo misk kwenye tupu zake na alale na udhu
Miski pia inazuia madudu mabaya kama vile Popobawa na majini Mahaba
Mtu mwenye kuwa anatokewa na mapopo bawa au majini Mahaba ajipake Miski katika tupu zake mbele na nyuma na mwili mzima kisha asome Ayat za kutoa uchawi na aya za kujilinda.Shuka atakayolalia aipake mafuta mazuri(Misk nyeupe) na chumba chake kifushwe ubani mweupe na asikilize Surat Baqarah na akithirishe kusoma Ayat Kursiyu kwa wingi , hakuna jinni au popobawa au mchawi atamfuata kwa Tawfiq ya Allah.

Suala la Muhimu na la Msingi
Yeyote yule atayenuia kuoa au kuolewa asome aya za kubatilisha uchawi na atumie Misk kama tulivyoeleza hapo mwanzo Allah atamlinda na mikosi na uchawi Bi-Idhni –Llah
na akithirishe kusoma dua zifuatazo
Siku atakapo-oa amshike mkewe kichwani na amsomee dua hii
Allahumma inni as’aluka khayraha wa khayra ma jabaltaha ‘alayhi wa a’udhu bika min sharriha wa shari ma jabaltaha’ alayhi. Allahumma baarik li fiha.
Kisha Surat Fatiha na Ayat Kursiyu huku akiwa amemshika kichwani

2. Siku atakayooa wasimame usiku na kuswali rakaa mbili au zaidi kumuomba Mungu awalinde na mabalaa ya kidunia(uchawi , hasadi,kijicho, majini nk) wafanye hivi kabla hawajaingiliana kimwili(jimai)
3.Wakiwa tayari kuingiliana na mkewe wasome Dua hii
Bismillahi Allahumma jannibna Al-Shaytaan wa jannib Al-Shaytaan ma razaqtana
4. Waendelee kuwa katika dhikr kila siku na kufanya Ibada za usiku mara kwa mara na wahudhurie sana kwenye madaira ya Dhikr na Hadhara
5.Wakithirishe kumswalia mtume sana
Allahuma swali ala Muhammadin wa Ala aali Muhamadin kama swalaita Aalaa Ibrahim wa alaa Aali Ibrahim wa barik alaa Muhammad wa aali Muhammadin kama Barakata alaa Ibrahima wa ala aali Ibrahim fil alamina innaka Hamidun Majiid

Mwenyezi Mungu atawakinga na balaa zote na atawajaalia mtoto mwema na mtiifu kwa wazazi wake kwa idhni ya AllahMke akipata Ujauzito na wakati mnapanga kuzaa
mama mjamzito kujilinda dhidi ya uadui, hasadi,majini na uchawi wakati akiwa mjamzito na dua za kuomba mtoto awe mwema , msikivu, mwerevu wa masomo na kadhalika……Aya hizi zinaweza kuandikwa kwenye karatasi kwa wino wa zaafarani na kuchanganywa na rose water na maji ya zamzam au maji yoyote masafi akapewa muhusika(yaani mama mja mzito) na kila siku asubuhi na jioni asome au asomewe ayah hizi, inapendeza mume akamsomea mkewe huku amemshika kitovuni kama msomaji sio mumewe basi amshike kichwani na vizuri zikarekodiwa hizi sura na Ayah akawa anasikiliza kila mara .Hii itakujaalieni kupata mtoto mwema, mtiifu, mwenye kipaji cha ajabu na pia itamfanya mzazi apate wepesi katika kuzaa na wakati wa ujauzito kwa idhni ya Allah.Na vyema zaidi mkaanza aamal hii kabla ya ujauzito kupatikana
Yaweza pia ayah hizi kuandikwa na kusomewa kwenye mafuta ya zaituni kwa kujipaka mzazi mtarajiwa.

Soma Surat Zilzalaha mara 11Surat Fussilat Aya 47
Ilayhi yuraddu AAilmu alssaAAati wama takhruju min thamaratin min akmamiha wama tahmilu min untha wala tadaAAu illa biAAilmihi

Surat Raad Aya ya 8
Allahu yaAAlamu ma tahmilu kullu untha wama taghiidu alarhamu wama tazdadu wakullu shayin AAindahu bimiqdarin“Surat Maryam

Aya 1 mpaka Aya ya 17Surat al-Naml 27:62
Dua hii ikhitimishwe kwa kusoma Hizbu Bahr na Hizbu Naswr na kumswalia Mtume kwa salawat yoyote ile yapendeza swalat Naria--- On Sat, 5/29/10, Manyaunyau Manyaunyau wrote:
From: Manyaunyau Manyaunyau Subject: Re:Dalili za kupatwa na JinniTo: "Abal Hakkam Liyasurutwiyah" Date: Saturday, May 29, 2010, 11:30 PM
nitumie picha yako na namba yako ya simu na picha za matukio ya kichawi na mengineyo--- On Sat, 5/29/10, Abal Hakkam Liyasurutwiyah wrote:
From: Abal Hakkam Liyasurutwiyah Subject: Re:Dalili za kupatwa na JinniTo: "Manyaunyau Manyaunyau" Date: Saturday, May 29, 2010, 10:51 AM

Dalili za kupatwa na Jinni

Dalili unapokuwa macho(ukiwa hujalala)
1.Kujisikia unachukia kufanya Ibada , kuchukia kufanya Dhikr
Angalia Quraan 43:36-37
2Kufanya makosa makosa katika kauli(maneno) , kutembea kwa kuangukaanguka2:275
3.Kuanguka kama kifafa bila ya kuwa na ugonjwa wa kuanguka kifafa nah ii ni moja katika dalili za kupatwa na jinni ima la kutupiwa au jinni la upepo mbaya(pepo mbaya)
4.Miguu kuwa haina nguvu(kupalalaizi) bila sababu maalum ya kitabibu
5 Kuwa na hasira bila sababu , au kulia bila sababu ya msingi
6.Kukaa chooni kwa muda mrefu na kuongea pekee yako na kujijibu
7Kuumwa kichwa mara kwa mara , na kichwa hakitulii hata ukinywa vidonge
8.Kwa upande wa wanawake kutokwa damu bila mpango maalum wa siku zao, angalizo katika hili kuna wanawake wenye Anemia wamuone daktari kwanza.
9.Kutokupata watoto, ingawa mume na mke wote ni wazima na wana uwezo wa kuzaa
Kuna dalili nyingi mno ila hizi ni katika hizo dalili

Dalili unapokuwa usingizini
1.Kupata ndoto za kutisha , ambazo zinakufanya kuona viumbe vya ajabu na vya kutisha, kujiona unaanguka toka ghorofani au unaanguka katika shimo, kuona nyoka usingizini.Kuota kuingiliana kimwili na mtu usiyemfahamu na kumuona mtu anakutisha usingizini

2.Kuwa msahaulifu , kuwa na wasiwasi, na kuwa muoga (unakuwa mwoga)wakati wa kuamka
3.Kuongea kwa sauti kubwa(kupayuka) ukiwa usingizini
Aya za kumsomea Mgonjwa aliyepatwa na jinni wa kutupiwa au jinni wa upepo mbaya(pepo) pia ayah hizi zinaandikwa kama Kombe kwenye karatasi safi na kulowekwa na kupewa mgonjwa kunywa na kujipaka mwilini kwa muda wa masiku ambayo tiba yake itakuwa ianendelea.Tiba hii ni kunywa , kujipaka na kusomewa.Aya hizi pia huweza kutumika kuweka kwenye mafuta ya Zaituni ili mgonjwa awe anajipaka

01.Surat Al-Fatiah 1:1-7
02. Surat Al-Baqarah 2:1-5
03.Surat Al-Baqarah 2:163-164
04. Surat Al-Baqarah 2:255-257
05. Surat Al-Baqarah 2:285-286
06.Surat Al-Imraan 3:18-19
07.Surat Al-A’raaf 7:54-56
08. Surat Al-Muminoon 23:115-118
09.Surat Al-Saffaat 37:1-10
10.Surat Al- Ahqaaf 46:29-32
11. Surat Al-Rahmaan 55:33-36
12. Surat Al-Hashr 59:21-24
13. Surat Al-Jinn 72:1-9
14. Surat Al-Humazah 104
15.Surat Al-Ikhlaas 112
16.Surat Al-Falaq 113
17. Surat An-Nas 114


Kujilinda nafsi yako dhidi ya uchawi na majini kwa kila siku
1.Sema Audhubillah Minashaitwani Rajiim
2.Soma Surat Al-Falaq na Surat An-Naas
3. Soma Ayat Al-Kursiy
4. Soma Surat Al-Baqarah yote
5. Soma vipande vya mwisho vya Surat Al-Baqarah
6.Soma Aya za mwanzo za surat Ghaafir
7.Soma Hizbu al Bahr, Hizbu Barr na Hizbu Nasr za Imam Abal Hassan As-Shadhili
8. Kithirisha kusema maneno haya
Laa ilaaha ill-Allah wahdahu laa shariika lahu, lahu’l-mulk wa lahu’l-hamd wa huwa ‘ala kulli shay’in qadiir

8. Fanya Dhikr muda mwingi na hudhuria daira za Dhikr na Hadhara kwenye misikiti ifanyayo dhikr kwa pamoja
9. Kuwa na udhu wakati wote na kuswali swala zako kwa Jamaa na kwa wakati

Aya za Kuwadhibu majini wa kichawi na majinni wa upepo mbaya(pepo)
01. Surat Al-Fatiah 1:1-7
02.Surat Baqara , Ayat Al-Kurisy 2:255
03.Surat Al-Nisa 4:167-173
04.Surat Al-Maa’idah 5:33-34
05. Surat Al-An’aam 6:93
06. Surat Al-A’raaf 7:44-51, 102-103
07. Surat Al-Anfaal 8:12-13
08. Surat Al-Tawbah 9:7
09. Surat Ibraheem 14:15-17, 42-52
10.Surat Al-Hijr 15:16-18
11.Surat Al-Isra’ 17:110-111
12. Surat Al-Anbiya’ 21:70
13.Surat Al-Dukhaan 44:43-52
14. Surat Al-Ahqaaf 46:29-34
15. SuratAl-Hajj 22:19-22
16.Surat Maryam 19:68-72
17.Surat Al-Mulk 67:5-11
18 Hizbu Bahr na Hizbu Nasr

0 comments:

 
Design by Kwetu Bongo